Jumanne , 17th Nov , 2020

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, ametangaza kifo cha Naibu Kamishna wa Polisi, Dhahiri Kidavashari kilichotokea leo katika Hospitali ya Christian Medical Center Trust (DCMCT) iliyopo, Dodoma ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Naibu Kamishna wa Polisi, Dhahiri Kidavashari wakati wa uhai wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya IGP Sirro, Kamanda Dhahiri Kidavashari, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Novemba, 17, 2020 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Aidha IGP Sirro, amesema kuwa msiba upo Kisasa huku taratibu za mazishi zikiwa zinaendelea wakishirikiana na familia ya marehemu.