Jumatatu , 21st Jun , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemuapisha Balozi Batilda Salha Burian kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora pamoja na Zuwena Omari Jiri kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.

Balozi Batilda Salha Burian akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Uapisho huo umefanyika leo Juni 21, 2021 Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali katika Nyanja mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu.

Akizungumza mara baada ya uapisho huo Waziri wa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amesema mmoja ya kazi aliyonayo Mkuu wa Mkoa mpya wa Tabora ni kuhakikisha halmashauri zinafanya vizuri kwani changamoto iliyopo katika mkoa huo ni ukusanyaji wa mapato katika halmshauri.

Balozi Batilda Salha Burian ameapishwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora leo ikulku Dodoma, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Ally Hapi ambaye alihamishiwa mkoa wa Mara.