#TANZIA Waziri Mstaafu afariki dunia

Wednesday , 6th Dec , 2017

Aliyekuwa Waziri wa Habari Mstaafu na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mstaafu, Mh. Joel Bendera amefariki dunia jioni ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho  Afisa Habari wa Muhimbili , Aminiel Eligaeshi amesema kwamba walipomkea Mh. Bendera majira ya saa 12:24 Mchana  akitokea Bagamoyo na amefariki  saa 4:03 jioni ambapo chanzo cha ugonjwa wake hakijawekwa wazi.

Akituma salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu Mh. Khamis Kagasheki amesema kwamba amepokea kwa mshtuko taarifa ya kifocha bendera na kwamba kipindi cha uhai wake marehemu alilitumikia taifa kwa jitihada kubwa.

"Nimepokea kwa mstuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndg Joel Bendera. Alilitumikia Taifa letu kwa jitihada kubwa. Kwa kutaja machache, aliwahi kuwa Mbunge, Naibu Waziri, Mkuu wa Mikoa kadha nk. Pole zangu kwa family, ndugu, rafiki,wa marehemu. Rest in peace Joel" Mh. Kagasheki.