Aunty Ezekiel akataa kumfuata Wema Sepetu

Jumatatu , 6th Jan , 2020

Muigizaji wa filamu nchini Aunty Ezekiel, amefunguka kuwa anapenda muonekano alionao rafiki yake Wema Sepetu, ila kwa upande wake amesema hana mpango wa kupungua kwa sababu ameridhika na jinsi alivyo.

Pichani ni Aunty Ezekiel akiwa na Wema Sepetu

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, mara baada ya kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari, Aunty Ezekiel amesema,

"Muonekano wake nauona upo poa, hata mimi naona nakaa kwa shida kwa sababu ya ubonge  kwa yeye alivyopungua nimependa, ila mimi sina mpango huo kwa kweli nipo poa kwa hivi nilivyo, kama kupungua labda iwe kidogo tu lakini kupungua zaidi sijawahi kuwaza" amesema Aunty Ezekiel.

Aidha Aunty Ezekiel akizungumzia hofu yake ya kupungua amesema,
"Sihofii chochote ila naamini mimi kama tayari ni mama wa mtoto, kwahiyo waswahili wanasema ukiingia leba kuna viungo lazima vibadilike, haviwezi kubaki vile vile na vitu vingine ukivilazimisha inakuwa shida, kwahiyo naukubali huu mwili ukizingatia bado nahitaji kuwa mama zaidi" ameongeza.