
Irene Uwoya
Uwoya ametoa vitisho hivyo leo kupitia ukurasa wake wa Instagram, lakini hajamtaja muhusika huyo ni nani.
''Kuna jirani yangu anapata tabu sana na maisha yangu, anaongea maneno mengi ohhh magari sio yake, oaahhh hana pesa, ohhh sijui nini, nataka nikwambie utapata tabu sanaaaaa, sababu uvionavyo ni rasharasha tu'', ameandika.
Mbali na hilo Uwoya ameongeza kuwa mtu huyo anayemfuatilia akae tayari kwani kuna mambo makubwa atayafanya kati ya tarehe 18 na 22 mwezi wa 12.
Hata hivyo hisia za juu ya maneno hayo kuwa yanamlenga Dogo Janja zimekuja baada ya Uwoya kusisitiza kuwa watu waache kuhusisha mambo yake na mtoto wa watu. ''Afu Acheni kumuhusisha mtoto wa watu na vitu visivyo muhusu'', ameandika.