Afariki kwa kuzidisha dawa za nguvu za kiume

Ijumaa , 26th Jun , 2020

Kutoka nchini Kenya, katika Kaunti ya Kakamega, mwanaume aliyejulikana kwa jina la Munala (42), amefariki Dunia baada ya kudaiwa kutumia dawa za Viagra ili kuongeza nguvu za kiume.

Akithibitisha taarifa hiyo Afisa kiongozi wa Polisi wa Kakamega David Kabena amesema, marehemu alikodisha chumba kimoja kwenye hoteli huku akiwa na mwanamke Anyango (31) siku ya Juni 23 mchana.

"Wawili hao waliagiza chakula katika hoteli hiyo ila mwanamke huyo ndiyo alikuwa amekula, asubuhi yake mwanamke huyo alitoka chumbani na kumfuata meneja wa hoteli na kumwambia kama mpenzi wake amefariki baada ya kutumia dawa za kupandisha ashiki za kimapenzi 'Viagra' kupita kiasi".

Afisa huyo wa Polisi ameongeza kusema "Mkuu wa hoteli hiyo aliwaita maafisa wa polisi, kisha kuupeleka mwili Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kaunti ya Kakamega ambapo ulifanyiwa upasuaji, na matokeo ya upasuaji yalionyesha marehemu alifariki kutokana na mshtuko wa moyo ambao unaaminika kusababishwa na dawa hizo".

Chanzo TukoNews, Kenya