Alhamisi , 22nd Jul , 2021

Huenda 2021 ukawa mwaka wa wasanii kuachia Album zao baada ya msanii wa HipHop kutoka Mji kasoro maji ya blue Stamina Shorwebwenzi kutangaza kwamba Album yake tayari imekamilika.

Msanii Stamina Shorwebwenzi

Via post yake ya Instagram Stamina ameandika kuwa "Kuna haja ya kuongea sana napokutana na wamemchokoza bear @bearbeatz_tz sisi tumemaliza kazi yetu bado kazi yenu ya masikio sasa, Album is done"

Mpaka sasa wasanii kama Dogo Janja, Weusi, Producer Abbah na Marco Chali wameshaachia Album zao sokoni na wengine waliotangaza kuja Album mwaka huu ni Alikiba, Diamond, Harmonize, Country Wizzy, Stamina, Ibraah, Killy Moni Centrozone.