Alikiba ametoa dukuduku lake kuhusu mapenzi

Jumanne , 7th Jan , 2020

Mfalme wa BongoFleva Alikiba, ametoa dukuduku lake kuhusu suala zima la mapenzi na kusema mapenzi yanaumiza na wala sio kitu cha mchezo mchezo.

Picha ya msanii Alikiba

Alikiba amesema hayo wakati akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, ambapo amezungumzia uzoefu wake kuhusu mapenzi na kama aliwahi kuimba wimbo wowote ambao uligusia uhalisia wa mapenzi yake.

"Ni kweli mapenzi yanaumiza na sio kitu cha mchezo mchezo, haina haja ya kusema kwamba umeumizwa kwenye mapenzi halafu unakaza watu watajua tu, mapenzi sijui kwanini yaani na mimi sitaki kujua, ila kiukweli mapenzi kavu sana hayafai" amesema Alikiba.

Aidha Alikiba ameongeza kusema, alishawahi kuandika wimbo kuhusu mapenzi na yaliyomkuta, ila hawezi kutaja ni wimbo gani ambao aliutoa kuhusiana na maisha yake ya mapenzi.