Jumatano , 21st Jul , 2021

Tegemea dude jipya kutoka kwa msanii Alalikiba kabla ya kuisha kwa mwezi Julai baada ya msanii huyo kudokeza ujio wa kazi yake mpya itakayoitwa jealous.

Picha ya msanii Alikiba

Kupitia page yake ya Instagram Alikiba ameandika kuwa "Before we continue with ‘bampa To bampa’ season, let me ask you ulishawahi kujiskia jealous kwenye kitu chochote"

Ngoma ya mwisho ya Alikiba inaitwa salute aliyoichia June 30 'ft' Rude Boy kutoka Nigeria hivyo anatimiza ahadi yake ya kuachia ngoma 'back to back' mpaka atakapoachia Album yake mpya na ya 3 kwenye maisha yake ya muziki mwezi August.