"Alikiba ni kama Jini" - K2ga

Jumatano , 8th Jan , 2020

Msanii wa kundi la "Kings Music" K2ga amesema alikuwa anatamani kujirekebisha asiimbe kama Alikiba lakini imeshindikana, pia anaona fahari kuambiwa anaimba kama Alikiba kwa sababu msanii huyo ni kama jini.

Kushoto kwenye picha ni K2ga, kulia ni Alikiba

Akipiga stori na e-Newz ya East Africa Television, ambayo inaruka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 12:00 jioni, K2ga amesema huwa anaambiwa anaimba kama Alikiba likini anaona hamfikii hata robo.

"Ukiambiwa unacheza mpira kama Ronaldo basi unajua na nashukuru Mungu kwa hilo, ni sahihi watu kuona naimba kama Alikiba kwa sababu kuna watu wanatamani kuimba kama yeye lakini wameshindwa, lakini mimi K2ga napita kama Alikiba ni sahihi kabisa" ameeleza K2ga.

Aidha K2ga ameongeza kwa kusema "Namtumia Alikiba kama mshauri na kila kitu changu ninachokifanya kwenye muziki  Alikiba ni kama jini, sijisifu kwamba naimba kama yeye kwa sababu sijamfikia hata robo au theluthi yake, mimi pia  natamani kuwa kama yeye".

K2ga ameachia audio na video ya wimbo wake mpya uitwao Unaniona.

Zaidi tazama Interview hapo chini.