Amber Lulu aeleza alivyoshea Mwanaume na Gigy

Jumatano , 9th Oct , 2019

Kwa kawaida siku ya Jumatano watu wameipendekeza kuita 'Woman Crush Wednesday', ambapo leo tumepiga stori na Amber Lulu, ambaye amefunguka suala la kushea Mwanaume na Gigy Money pamoja na wanawake kupenda pesa.

Amber Lulu na Gigy Money

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, kuhusu kugombania mwanaume na Gigy Money, Amber Lulu amekiri kuwa alishawahi kushea mwanaume mmoja kipindi cha huko nyuma.

"Kutokana na 'Lifestyle' ya sasa hivi watu hawamjui bwana angu kwa hiyo wanajitahidi kumtafuta na kuotea kama natoka na nani, mimi sijawahi kugombana na mtu hizo stori za kugombania mwanaume ni zamani sana, kama miaka mitatu au miwili nyuma huko , nakumbuka mwanaume ambaye mimi nilipita na yeye alipita ni Casto Dickson'' amesema Amber Lulu.

Aidha msanii huyo amezungumzia suala la wanawake kudanga ili wapate pesa, ambapo amesema kuwa.

"Inatokeaga mara nyingi sana, Bongo hakuna mwanamke awe na mtu halafu akatae pesa, kila mtu anategemea mwanaume mwenye pesa, halafu sisi wanawake tunapenda kupewa ila inategemea unadanga kiasi gani" amesema Amber Lulu.