Amber Rutty amtongoza mumewe kwa Kiingereza

Alhamisi , 7th Nov , 2019

Kupitia EATV & EA Radio Digital, tumewapata Amber Rutty na mume wake aitwaye Davil, ambapo siku ya leo wameamua kutuletea vituko vya kutongozana kwa kutumia Lugha ya Kiingereza.

Mazungumzo yao yalianzia kwenye gharama za mavazi na mionekano, ambapo Amber Rutty amesema rangi aliyopaka nywele zake, gharama yake ni kiasi cha Shilingi milioni 3, na Lipstick yake inatoka Marekani kwa 'role model' wake Amber Rose.

"Mimi sijichubui, nywele zangu natengengeneza kwa milioni 3, Lipstick yangu mara nyingi naipata kutoka kwa 'role model' wangu Amber Rose, huwaga ananitumia na ananipaga punguzo la bei kwa Shilingi laki tano, mume wangu ndiyo anagharamia pesa zote hizo" amesema Amber Rutty.

Pia Amber Rutty amesema, kitu anachokipenda kwa mume wake Davil ni vinyweleo vikubwa alivyonavyo kwa sababu vinamkosha na kumtekenya.