Amber Rutty na mumewe waa-update ndoa yao

Jumapili , 21st Jun , 2020

Msanii Amber Rutty ame-update ndoa yake na mumewe Davil baada ya kuachana kwa muda mrefu kisha kutalakiana kwa talaka iliyodumu kwa muda wa miezi miwili na nusu.

Amber Rutty na mumewe Davil Tz

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital Amber Rutty amesema wameamua ku-update ndoa  na mahusiano yao kwa sababu kulitokea malumbano na walishindwa kuelewana na sasa hivi wamerudiana tena.

"Siku ya jana tulikuwa tuna update mahusiano yetu tangu tulivyofunga ndoa hapo katikati kulitokea malumbano, kushindwana kuelewana na tukafarakana ila sasa tumerudiana, kwa hiyo mume wangu ameamua kua-update kwa kusheherekea ili mahusiano yetu yawe mapya kabisa na alinifanyia suprise ya kunivalisha pete" amesema Amber Rutty 

Ziadi tazama tukio kamili hapa chini.