Amber Ruty acheza utupu jukwaani

Jumatatu , 18th Mar , 2019

Video Vixen, Amber Ruty ambaye hapo jana ameanza ku 'trend' kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa video akiwa mtupu jukwaani, amefunguka juu ya tukio hilo la aibu, na kusema ni pombe ndio zimepelekea kufanya vile na kamwe hawezi kuvaa tena vazi kama lile.

Akizungumza na www.eatv.tv  Amber Ruty amesema mambo yote aliyoyafanya yalitokana na pombe, na hata nguo aliyovaa iliyomuacha wazi baadha ya sehemu za siri zikionekana, hakuivaa.

Amber Ruty mwenyewe ajitetea

“Mimi nilikuwa nimelewa, mimi sikuvaa zile nguo nilivyotoka nyumbani, tulivyoenda club kwenye saa 8 au saa tisa ndio nikajikuta nimevaa nguo ile, na siwezi kuvaa nguo kama zile kwenye maisha yangu yote, sijui nisemeje, kwa kifupi siko sawa”, amesema Amber Ruty.

Ikumbukwe kuwa video vixen huyo tayari ana kesi mahakamani ambayo anaweza akafungwa miaka 30 jela, iwapo atakutwa na hatia, baada ya kuvuja kwa video zake zikimuonesa akiingiliwa kinyume na maumbile, na mpenzi wake Saidi Mtopali jambo ambalo ni kinyume na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.