Ijumaa , 22nd Oct , 2021

Mwigizaji wa filamu na mchekeshaji kutoka nchini marekani , Alexander Rae Baldwin, mwenye umri wa miaka 68

Picha ya Mwigizaji Alexander Rae Baldwin

Anashikiliwa na polisi mara baada ya kufyatua risasi kwa bahati mbaya na kumuua director wa filamu, Halyna Hutchins (42) pamoja na kuwajeruhi wasaidizi wake  wakati wakiwa kwenye seti ya filamu mpya ya  “RUST” ambayo  inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Kutokana na uchunguzi uliofanyika  inaonesha kuwa “script” ya filamu hiyo  ilihusisha matumizi ya bunduki, hivyo haikubainika mara moja ikiwa bunduki iliyomuua director Hutchins ilikuwa imebeba risasi halisi au bandia.