"Baba yetu alituzaa 46,kwa wake tofauti" - Timbulo

Jumanne , 30th Jun , 2020

Msanii wa BongoFleva Timbulo amefunguka kuwa huwa anamuona baba yake kama babu yake kwa sababu kwao wamezaliwa watoto wengi sana hadi kufikia hatua ya mzazi wake huyo kuwachanganya na watoto wengine.

Msanii wa BongoFleva Timbulo

Timbulo amesema kwao walizaliwa jumla ya watoto 46 kwa mama tofauti japo wengine wameshafariki, baba yake alikuwa na wake wanne na kwa upande wa mama yake yeye ni mtoto wa mwisho kati ya 13 waliozaliwa baba mmoja na mama mmoja.

"Baba yangu alikuwa na watoto wengi hadi kuna muda alikuwa anatuchanganya, tulizaliwa 46 kwa wake zake wanne tofauti, mimi mpaka najitambua tulikuwa tupo 34 japo kuna wengine walitangulia mbele za haki, mimi kwa upande wa mama yangu tulizaliwa watoto 13 na mimi ndiyo nilikuwa wa mwisho, mimi naona kama ni mjukuu kwa baba yangu kwa sababu alikuwa amezeeka" ameeleza Timbulo