Alhamisi , 21st Jan , 2016

Star wa muziki Baby J anayetokea visiwani Zanzibar anatarajia kuonesha uwezo wake mkubwa wa kurekodi kwa kuzirudia nyimbo za aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab Fatuma Bint Mbaraka almaarufu kwa jina la Bi Kidude.

Staa wa muziki Baby J kutoka visiwani Zanzibar

Baby J ameiambia eNewz kuwa wazo hilo limemjia kutokana na jinsi alivyomfahamu na kuishi na gwiji huyo akijiandaa kuingia studio akishirikiana na producer Shirko katika kurekodi nyimbo maarufu za Bibi Kidude zikiwemo 'Muhogo wa Jangombe' na 'Kijiti' lengo kubwa ni kumuenzi gwiji huyo.