Jumapili , 21st Jan , 2024

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), limeyataka makampuni yanayoendesha mashindano ya urembo nchini kufata sheria, Kanuni na taratibu za mashindano ili kuweza kutenda haki kwa washiriki ili kuondoa manung’uniko ya upendeleo pamoja na kupanda mshindi anaestahili.

Hayo yamesemwa na Afisa Sanaa mwandamizi kutoka BASATA, wakati anazindua shindano la Miss Kinondoni 2024, Jana January 20 na kuwasisitiza waandaaji kuzingatia maadili pia kwenye mashindano hayo ili kuweza kutoa viongozi ambao watakuja kuisimamia jamii kikamilifu.

Kwa upande wake muandaaji wa mashindano hayo Queen Johnson anasema kauli mbiu ya mwaka huu ni urembo na uongozi hivyo wamejiandaa kuendesha mashindano yatakayozingatia maadili kwa warembo watakaojitokeza ili baadae wanapoaminiwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi waweze kuisimamia jamii kwa usahihi.