Jumanne , 3rd Sep , 2019

Justin Bieber Kupitia akaunti yake ya Instagram, ameandika changamoto kadhaa alizopitia na zaidi akishukuru ndoa yake kwa kusema imemsaidia kumfanya awe mpya.

Katika Post' yake Justin ameandika namna alivyopambana kwa kuishi na wazazi wake wote wawili ambao walitengana akiwa bado mdogo, maisha ya usupastaa', matumizi makubwa ya madawa ya kulevya akiwa na miaka 19 na kutokuwa na heshima na hasira kwa wanawake kipindi akiwa katika mahusiano yake kadhaa ya nyuma.

"Nilitumia miaka kadhaa ili kuweza kurudi kuwa mpya kwa kurekebisha mahusiano yangu kadhaa, kubadilisha tabia ya mahusiano yangu nashukuru Mungu sasa nimezungukwa na watu ambao wananipenda  na zaidi nipo nasafiri katika kipindi bora cha maisha yangu Ndoa," aliandika.

Justin Bieber na Mchumba wake Hailey Baldwin kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinaonesha wawili hao tayari ni wanandoa, lakini hakuna uthibitisho uliotolewa kati yao kuhusu suala hilo.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Hope you find time to read this it’s from my heart

A post shared by Justin Bieber (@justinbieber) on