Ijumaa , 22nd Oct , 2021

Rapa Big Sean kutoka nchini Marekani ameshea picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa na kundi la nyuki wakati ana shoot video yake mpya ya “What A Life”, Big Sean anadai kwamba nyuki hao walikuwa Elfu 65,000 mwilini mwake.

Picha ya Big Sean akiwa na nyuki hao Elfu 65

Big Sean ameongeza kusema alikuwa na upendo kwa mzinga wa nyuki, na hataki kufikiria suala hilo kama lilikuwa na athari kwake au ujinga.