Bright afunguka sababu ya kutomiliki gari 

Alhamisi , 6th Dec , 2018

Msanii anayefanya vizuri hivi sasa kwenye gemu ya Bongo Fleva, Bright amefunguka sababu ya kutomiliki gari hadi hivi sasa licha ya kupata umaarufu kupitia kazi hiyo.

Bright

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Jumatatu hadi Ijumaa, Bright amesema kuwa umaarufu wake umeongezeka kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka iliyopita lakini bado hajayaona matunda ya umaarufu huo.

"Bright wa sasa sio wa miaka iliyopita, lakini umaarufu nilionao hauendani na ninachokipata. Bado sijapata hela kubwa kiasi hicho, kiasi kwamba naweza kununua gari," amesema.

Pia msanii huyo amezungumzia juu ya mgogoro dhidi ya 'Management' yake ya Fundikira kuwa hawana maelewano mazuri yaliyompelekea kufanya kazi zake mwenyewe.

"Sitopenda sana kuzungumzia vitu hivyo lakinia kumekuwa na vitu mbavyo haviendi sawa ndiyo maana kumekuwa na taarifa hizo. Mimi na Management yangu tutakaa na kutoa taarifa rasmi," ameongeza.

Bright ametambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Shotoa'.