
Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Television, amesema ingawa kitendo hiko sio kizuri na hatari kwa usalama wake, lakini karibia mwaka mzima huu wa 2017 hajawahi kutumia condom.
"Hilo suala kila siku namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie, tangu huu mwaka uanze sijavaa kondom, mimi kama mfano wa kuigwa siko kakma kupotosha watu, nakiri huu mwaka unaisha, tunasema vitu ambavyo tumekosea na kujifunza, lakini sitarudia tena hayo makosa sababu hayo makosa, inshallah mwakani nitaanza", amesema Calisah.
Hivi karibuni mwanamitindo huyo alishatangaza kufungua duka la kutia ujauzito wanawake kwa yeyote atakayehitaji kuzaa na yeye.