CHEKA TU wazungumzia kifo cha mchekeshaji Martha

Jumatano , 11th Sep , 2019

Uongozi wa CHEKA TU umezungumzia kuhusu taarifa ya kifo cha mchekeshaji Martha Shilole kilichotokea Asubuhi ya leo Jijini Dar es Salaam.

Martha

Kupitia kwa mmoja wa wasanii wa vichekesho hivyo ambavyo huruka kupitia EATV, amesema kuwa wenyewe wameshtushwa na taarifa ya kifo hicho kwakuwa hawakutarajia  kutokana na kuugua kwake ghafla.

"Ndugu Martha ametutoka leo Alfajiri na maeneo alipokuwa akiuguziwa ni huku Kivule Majohe ambako alikuwa akiuguzwa na wanafamilia wake. Tunachosubiria sasa ni baba yake afike ili taratibu za mazishi zifanyike", amesema msanii huyo ambaye alikuwa akisimama jukwaa moja na Martha.

"Walikuwa wanawake wawili tu pale CHEKA TU, mmoja ndiye huyu ametutoka kwahiyo ni pigo kubwa sana kwetu watazamaji wetu wanaotuangalia", ameongeza.

Taarifa za kifo cha Martha zimesambaa mchana wa leo ambapo inaelezwa kuwa alikuwa akiugua homa kali.