Jumatano , 11th Dec , 2019

Msanii wa filamu nchini, Chuchu Hansy, amekanusha madai ya yeye kulindwa na silaha na mpenzi wake, ambaye pia ni mzazi mwenziye, Vincent Kigosi maarufu kama Ray.

Muigizaji wa filamu nchini, Chuchu Hansy.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Chuchu Hansy amesema hawezi kuliongelea suala hilo kwa sababu Ray ni Baba wa mtoto wake na ana maisha yake na vitu vyake vingine hawezi kuvizungumzia.

"Siwezi kumuongelea kwa sababu ana vitu vyake, vingine ambavyo siwezi kuvizungumzia ni vizuri mkimuona mumuulize hilo swali, kama anayo au hana atawaonesha, sisi Watanzania hatuna desturi ya kulindana, hivyo nitaishi maisha ambayo Nchi yangu inaruhusu" amesema Chuchu Hansy.

Aidha Chuchu Hansy ameongeza kuwa "Siwezi kulindwa kwa sababu mimi sijafikia hatua ya kulindwa na silaha, mtu akiamua kufanya jambo au kitu chake anafanya tu hata ulindwe kwa saa 24 atafanya tu ndani ya dakika hata 5 au sekunde".