Jumamosi , 30th Jul , 2016

Shindano la Dance100 leo limeingia katika usaili wake wa mwisho katika viwanja vya TCC Chang’ombe Jijini Dar es salaam ambapo jumla ya makundi 25 kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam yamejitokeza kushiriki shindano hilo.

Kundi la Best Boys lilipokuwa likionyesha ufundi wa kucheza TCC Chang'ombe.

Akizungumza na EATV mmoja wa majaji wa shindano hilo Super Nyamwela amesema uwepo wa makundi 25 imeonyesha kuwa watu wengi walikuwa wanasubiria siku ya leo kwa hamu ili waweze kuonyesha vipaji vyao jambo ambalo limefanikiwa na mamia ya mashabiki wa Dance100 kujitokeza kwa wingi kushuhudia.

‘’Leo ni usaili wa mwisho ndiyo maana maana makundi yamevunja rekodi kwa kujiandikisha 25 ambapo usaili wa kwanza yalijitokeza makundi 10, usaili wa pili 21 na wa leo yamejitokeza makundi 25 jambo ambalo ni la kujivunia kwamba vijana wanazidi kutambua umuhimu wa shindano’’-Amesema Jaji Nyamwela.

Baada ya mchuano huo mkali wa siku ya leo makundi matano yameweza kuibuka kidedea katika kusonga mbele na shindano makundi hayo ni P.O.D Crew, Ikulu Vegaz, Clever Boys, Best Boys, na Timu Makorokocho .

Tags: