Jumatatu , 2nd Feb , 2015

Akiwa amejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka huu, msanii wa muziki Dyna ametoa kauli ya matumaini kwa mashabiki wake kutarajia ujio wa project kubwa kutoka kwake na wasanii wanaofanya vizuri hapa Afrika Mashariki.

msanii wa muziki wa bongofleva Dayna Nyange

Dayna amesema kuwa, katika sanaa ili kufanya mambo makubwa inahitaji kuanza na hatua za awali kwanza, akiahidi kulishika soko la Afrika Mashariki kabla ya kwenda mbali zaidi.