Jumamosi , 20th Jan , 2024

DJ Seven Worldwide amenyoosha maelezo kinachoendelea kati yake na Harmonize baada ya taarifa kwamba sasa hivi hawafanyi kazi pamoja baada ya msanii huyo kuanzisha mahusiano na mrembo Poshy Queen.

Picha ya DJ Seven

Kupitia Mahakama Kuu ya Burudani Friday Night Live DJ Seven amesema “Mimi sio DJ wa Harmonize tena, ni muda kidogo umepita wiki 2 au 3 hivi.Kuhusu Poshy Queen naomba tumuache sasa hivi sina mahusiano tena”.

Inasemekana Harmonize ameanzisha mahusiano na Poshy Queen ambaye kipindi cha nyuma alikuwa mpenzi wa DJ wake Seven.