Ijumaa , 20th Jun , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Dr. Hilderman amewaomba radhi waamini wa dini ya kikristo nchini Uganda, baada ya kitendo chake cha kutumia mavazi maalum yanayovaliwa na maaskofu.

Msanii wa Uganda Dr. Hilderman

Kitendo hiki cha Dr. Hilderman kutumbuiza na mavazi hayo jukwaani kimetafsiriwa kama kufuru ya aina yake na kimemuweka matatani msanii huyu ambaye amejitetea kuwa, hakuwa na nia ya kushusha heshima wala hadhi ya mavazi hayo.

Akiwa anazindua albam yake inayokwenda kwa jina la Sinze Ya Leeta Enaku, Dr. Hilderman amezua mkanganyiko mkubwa baada ya kupanda jukwaani na mavazi haya ya kidini na kuanza kugawa baraka kwa mashabiki wake kama vile wafanyavyo wahubiri.