Jumanne , 11th Jan , 2022

Baby Mama wa msanii Rayvanny Fahyma 'Fahyvanny' amevunja ukimya wa kushochwa na story zinazosemekana mitandaoni kwamba ameachwa kwenye mahusiano yake.

Picha ya Fahyma

Fahyma ametoa dukuduku hilo kwenye 'Insta Story' yake kwa kuandika ujumbe ufuatao kwa wanaomdhihaki kwamba ameachwa.

"Nasema hivi mnikome jamani Fahyma kaachwa kaachwa, nimechoka na kama sijaachwa je? na wewe unayeendelea kunichokonoa endelea kuna jambo unalitaka".