Alhamisi , 29th Feb , 2024

Mwanamuziki wa Nigeria, Adedamola Adefolahan maarufu kama Fireboy DML, ameukosoa muziki wa Afrobeats nchini humo akisema kuwa ni muziki usiojali maudhui (uandishi) na badala yake unabebwa na ‘vibes’ zaidi. 

 

Akiwakosoa wasanii wengine wanaofanya muziki wa Afrobeats, katika mahojiano ya hivi karibuni na Billboard News, mkali huyo wa ‘Vibration’ ameongeza kwamba kwa kiasi kikubwa Afrobeats imeshindwa kugusa maisha halisi ya watu kwasababu umekuwa ni muziki wa kuchezeka (klabu) zaidi kuliko kuibua hisia za ndani za watu wanaosikiliza muziki huo

'Tangu mwanzo Afrobeats ilijengewa misingi ya vibes, hata mimi niligundua kuna kitu kimekosekana, hakuna uandishi, hakuna ushairi, ni vibes tu, inachosha sana’ - Fireboy DML.