Alhamisi , 26th Aug , 2021

Msanii wa BongoFlava Foby ameeleza hisia zake za kumpenda mchekeshaji Ebitoke mpaka amefikia hatua ya kumuweka kwenye 'Profile picture' kwenye akaunti yake ya Instagram.

Msanii Foby kushoto kulia ni Ebitoke

Akipiga story na Planet Bongo ya East Africa Radio, Foby anasema sababu za kumuweka Ebitoke kwenye 'Profile' yake ni kumuelewa na kumkubali mshekeshaji huyo.

"Nampenda muda mrefu sana, napenda uigizaji wake kuna vitu fulani ananikumbusha nikiwa mtoto ili uchekeshe lazima ujipake vitu usoni hivyo napenda kitu anachofanya ndio nikaamua nimuweke profile sidhani hata kama yeye anajua" amesema Foby

Aidha Ebitoke naye alishawahi kuweka hisia zake kwa msanii Ben Pol na sasa hivi anaonyesha kumkubali zaidi msanii Alikiba.