Alhamisi , 26th Jun , 2014

Msanii wa muziki Size 8 kutoka nchini Kenya, ametenga muda wake kusaidia wakazi wa huko Murang'a nchini Kenya ambao wanasumbuliwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la funza.

Msanii wa nchini Kenya Size 8

Katika shughuli hii, Size 8 mbali na kushiriki katika shughuli ya kuwatoa baadhi ya wakazi hawa funza katika miguu yao, pia alitumia muda wake kutoa burudani na pia kugawa pea za viatu kwa wanafunzi katika shule ya msingi Gatanga iliyopo huko Murang'a.

Katika kazi hii Size 8 ameshirikiana na watu wengine maarufu katika tasnia ya burudani Kenya, akiwepo mchekeshaji mahiri anayefahamika kwa jina Jalang’o.