
Kushoto ni Madam Rita, kulia ni Harmonize
EATV & EA Radio Digital imepiga stori na Boss wa mashindano hayo ya BSS Madam Rita na amenyoosha maelezo jinsi ilivyotokea kwa kipindi kile hadi kufikia hatua ya kutompitisha kwenye mashindano hayo.
"Hatuna tatizo naye, ni msanii mzuri ila kipindi kile alivyopita alikuwa hajajiandaa sio kwamba tulimchukulia poa na tulikuwa hatumjui wala hatukumfanyia makusudi ila ni mambo ya kawaida na tunamkubali, tunafurahia anavyong'aa kwa sababu alipita pale, sekunde 30 huwezi ukaona kipaji cha mtu ila baada ya muda unaweza ukaona" ameeleza Madam Rita
Zaidi tazama kwenye video hapa chini