Jumatano , 21st Jul , 2021

Mfalme wa Temeke Young Tuso amefunguka kusema Harmonize alimkatisha tamaa baada ya ku-date na staa wa filamu Jacqueline Wolper kwa sababu hata yeye alitamani kuwa naye kwenye mahusiano.

Picha ya Young Tuso na Harmonize

Young Tuso ambaye alishamuandikia hadi wimbo Jacqueline Wolper wa kumsifia na kumshawishi kuwa naye kwenye mahusiano anasema mwanzo alidhani Harmonize na Wolper wanatania ila baadae ikawa serious.

"Ilivyofika suala la Wolper kuwa na mahusiano na Harmonize ilikuwa KO kubwa kwangu, nilijia watu wanamtengeneza Harmonize awe mkubwa kwa kipindi kile ila ilinichanganya k uona Wolper kaenda hadi kusini kwa Konde Boy mara anapika na mama yake Harmonize nikaamini wapo serious"

"Konde Boy alinikatisha sana tamaa kwenye movement zangu za kumpata Jacqueline Wolper, roho ilikuwa inaniuma na kunichanganya sana" ameeleza Young Tuso

Zaidi fuatilia hapo chini kwenye video akizungumzia hilo.