'Sijakutana kimwili tangu nizaliwe' - Dorah

Ijumaa , 4th Oct , 2019

Muigizaji wa Tamthilia hapa nchini anayejulikana kwa jina la Dorah, amesema kuwa kwasasa yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume anayefahamika kwa jina la Edson, na wamedumu kwa muda wa miaka 5, lakini hawajawahi kukutana kimwili.

Dorah ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwene kipindi cha Kikaangoni, kinachorushwa kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana, kwenye kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV.

''Nina miaka 24, mimi ni bikra, sijui kabisa mambo ya mapenzi, mpenzi wangu anaitwa Edson, tupo kwenye mahusiano mwaka wa tano sasa, lakini hatujawahi kukutana kimwili" amesema Dorah.

"Sijawahi kutishiwa kuachwa kwenye mapenzi ila mimi huwa namtisha kila mara mpenzi wangu" amesema Dorah.

Tazama mahojiano kamili.