Alhamisi , 11th Jun , 2020

Kufuatia madai ya kublokiwa kwenye mtandao wa Instagram na msanii Harmonize,  Harmorapa amekataa kumuomba msamaha ili kwenda sawa, kwa kusema suala hilo haliwezi kutokea kwani hakuna jambo ambalo amemkosea.

Kushoto pichani ni Harmorapa, kulia ni Harmonize

Akizungumza kwenye mahojiano ya EATV & EA Radio Digital, Harmorapa amesema kuwa suala la kublokiwa na Harmonize lina stori ndefu na hawezi kulizungumzia kwa sasa ila ikifika muda ataweka wazi kila kitu.

"Siwezi kukaa kumuomba msamaha kwa sababu, sidhani kama kuna jambo nimemkosea, kwanza kila mtu ananyota yake na siwezi kutembelea nyota ya mtu, Mungu aliyeniumba mimi ndiyo kamuumba yeye na watu wote,  kwahiyo haiwezi kutokea kumuomba msamaha kisa nimetembelea nyota yake na sijamkosea kama ningemkosea ningemuomba msamaha, hata mimi nilikuwa na upepo wangu" ameeleza Harmorapa 

Zaidi tazama kwenye mahojiano ya video hapo chini.