Alhamisi , 26th Jun , 2014

Baada ya kazi ambayo inakwenda kwa jina Mimi na Wewe kutoka kwa Dyna kufanya vizuri katika chati za muziki mbalimbali ndani na nje ya Afrika Mashariki, mwanadada huyu kwa sasa amejipanga vyema kwa ajili ya ujio mpya.

Msanii wa bongo fleva Diana Nyange

Diana ameiambia enewz kuwa rekodi hiyo mpya ambayo inakwenda kwa jina 'I DO' ataiachia siku ya kesho huku akiwasihi mashabiki wake wake mkao wa kula kuipokea kazi hiyo mpya.

Dyna amesema kuwa, kazi hii imetayarishwa na prodyuza mkali Triss na ni zawadi nyingine matata kwa mashabiki wake ambao siku zote amekuwa akijituma kwa ajili ya kuwatengenezea kazi na burudani nzuri kupitia muziki wake.

Kuhusiana na kazi hii, Dyna hapa anafunguka mwenyewe.