Jumatatu , 2nd Sep , 2019

Staa wa filamu Jacqueline Wolper, amefunguka kuhusu suala la kudanga kwa wanawake, na 'issue' za kutumika kwa warembo katika tasnia ya filamu.

Jacqueline Wolper

Jacqueline Wolper ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa filamu ya Siyabonga ya msanii Gabo Zigamba, uliofanyika Mlimani City, Jijini Dar es salaam.

Kuhusu suala la kudanga Wolper ameiambia EATV & EA Radio Digital kuwa, ''mimi ndiyo tayari nilishawahi kudanga, kwa kawaida kudanga ninavyoijua na nivyoielewa maana yake ni kuwa na mahusiano na mwanaume mwenye pesa, hiyo maana nyingine wanayoijua wao mimi siijui".

Aidha Wolper ameendelea kuzungumzia suala la wanawake wakiwa warembo wanaingia katika filamu bila ya kuwa na kipaji.

"Tunawalaumu watayarishaji na waongozaji wa filamu maana wanataka kuwakaza halafu ndiyo wawape majukumu, kama mtu amechukuliwa kwa ajili ya urembo na sanaa yake haijulikani hawezi kuendelea kupewa kazi".

Pia amesema wanawake hao wanaishia kuchezewa na kutumiwa hawawezi kuchukuliwa na watu wenye taaluma zao.

Mwisho amemaliza kwa kusema uzuri na ubaya wa tasnia ya filamu huwa ni kazi moja huanzisha nyingine.