Jumanne , 18th Dec , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Kenya, Eliud Sagini maarufu kama Sagini, amefariki dunia muda mchache baada ya kufikishwa hospitali kwaajili ya kupatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimetolewa na rafiki kipenzi wa msanii huyo, Khaligraph Jones, ambapo aliandika kwenye ukurasa wake wa instagram kuwa kifo chake kimetokea jana Desemba 17 baad ya kuugua kwa muda mfupi.
 

Wakati wa uhai wake Sagini ameshafanya kazi mbalimbali za muziki, zikiwemo alizoshirikiana na wasanii wakali kama Khaligraph Jones na rapper Young Killer wa hapa bongo.