Jinsi Foby alivyopata 'demu' kiulaini

Jumatatu , 9th Sep , 2019

Mkali wa BongoFleva Foby ameeleza sababu zilizomfanya apate 'demu' kisa umahiri wake wa kucheza mchezo wa mpira wa kikapu na mpira wa miguu.

Foby (kushoto)

Foby ameeleza hayo katika hatua ya 16 bora kwenye mashindano ya Sprite Bball Kings 2019, iliyofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili iliyopita katika viwanja vya Don Bosco, Osterbay.

Kuhusu kupata 'demu' Foby ameiambia EATV & EA Radio Digital kuwa,

"Kuna manzi nilishawahi kumpata mkoani kwetu, unajua michezo inawaweka watu karibu, mimi nilikuwa nafanya  mambo ya muziki na mpira, nilivyomfuata wala haikuleta shida yoyote tukabadilishana namba baada ya hapo 'fresh' mambo mengine yakaendelea".

Aidha Foby ameeleza kitu anachovutiwa nacho kwenye mashindano ya Sprite Bball Kings 2019 ambapo amesema,

"Mimi ni mwanamichezo napenda sana michezo, mpira wa kikapu naupenda sana isipokuwa mwili wangu ulinifanya nisicheze ila naelewa kila kitu ndiyo maana kila mwaka siwezi kukosa".

Pia amesema mashindano ya Sprite Bball Kings 2019 yatakuwa magumu sana na kila timu ipo vizuri ila timu anayoishabikia na kuvutiwa nayo ni Mchenga Bball Stars.