Jumamosi , 16th Mei , 2020

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amemaliza bifu na kuwapa ushauri wanamitindo Calisah na Ben Breaker pia amesema ameilewa ngoma mpya ya kundi la Rostam "kaka tuchati".

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza

Akizungumza kwa njia ya simu kupitia show ya "Friday Night Live" ya East Africa TV, Naibu Waziri alianza kuwapa ushauri wanamitindo hao ambao walikuwa wana bifu siku za nyuma, kisha akamalizia kwa kusema ameilewa ngoma ya kaka tuchati.

"Niwapongeze kwa kuwakutanisha hao vijana wetu wawili, nafikiri sisi kama Wizara ambayo tunasimamia kazi za sanaa naona tasnia ya ubunifu na uwanamitindo bado ni changa hapa kwetu na inakua, kwa hiyo waliokuwepo wanahitaji kuunganisha nguvu ya pamoja ndiyo maana nikawasisitiza huu sio wakati wa malumbano na kuangalia nani mkubwa nani mdogo" ameeleza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo

Aidha katikati ya mahojiano hayo akamalizia kwa kusema msalimie Stamina namuona hapo, goma nimelielewa sana kaka tuchat. 

Mahojiano kamili tazama kwenye video hapa chini.