Jumatatu , 27th Apr , 2015

Staa wa muziki kutoka bendi ya Twanga Pepeta, Kalala Junior ameweka wazi juu ya mipango ya ujio wa kishindo katika game ya muziki akiwa kama msanii binafsi, akiwa sasa amepata msimamizi atakayekuwa anasaidia kuendesha kazi zake.

mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta Kalala Jr

Kalala pia ameweka wazi juu ya kuwekeza katika rekodi aliyofanya na wasanii wa Bongo Flava, Makomandoo, akiwa na mpango wa kusafiri kwenda Nigeria kufanya video ya kazi hiyo.