Alhamisi , 21st Oct , 2021

Mwanasheria Steve Greenberg anayefanya kazi na mwimbaji wa RnB, R. Kelly amethibitisha kuwa Kells aliwekewa uangalizi wa kina akiwa gerezani baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya kujihusisha na biashara ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia kwa hofu ya kujiua.

Picha ya mwimbaji wa RnB, R. Kelly

Hivi sasa hatua hiyo imeondolewa ila baada ya kukutwa na hatia hukumu yake inatarajiwa kusomwa mapema mwezi Mei 2022 ambapo inaelezwa kuwa anaweza pigwa nyundo kuanzia miaka 10 hadi kifungo cha maisha gerezani.