Kimeumana, Nay na Baby mama wake wapeana makavu

Jumatatu , 10th Mei , 2021

Ni headlines za msanii Nay wa Mitego na mama wa mtoto wake Skyner Huniz ambapo siku ya leo wametupiana vijembe kupitia mtandao wa Instagram.

Nay wa Mitego na Baby Mama wake Skyner Huniz

Vijembe hivyo vimeanza baada ya Nay wa Mitego kumjibu shabiki kwamba hawezi ku-deal na mwanamke ambaye kilaza na mvuta bangi akiwa anamaanisha ni mama wa mtoto wake Skyner Huniz.

Baada ya muda mama wa mtoto wake huyo aliweka ujumbe ambao unaeleza kwamba Nay wa Mitego alipe ada ya mtoto kwanza la sivyo ataongea mambo mengine ya kumdhalilisha.

"Nimekuwa mvuta bangi leo hii daah, Mwanaume mwenye akili timamu hakimbii majukumu kwa mwanae wa damu, kwanini ada ya mtoto izue balaa lipa ada kabla sijachukua sheria, nikiamua kufungua huu mdomo utadhalilika, mimi ni kobe nimeinama nikinyanyua kichwa nikianza mwendo tusilaumiane" ujumbe wa Skyner Huniz 

Maneno hayakuishia hapo kwani Nay wa Mitego akajibu kupitia Insta Story yake kwa kuandika "Mwanamke anayejitambua hawezi kuweka matatizo ya kifamilia kwenye mitandao, unayenilalamikia nilipe ada umeni-block sasa napataje ujumbe wako, ina maanisha watu wa Instagram ndio walipe ada ya mwano, ushauri wangu nenda Mahakamani achana na mitandao"