Jumatano , 19th Jun , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdu Kiba, amefunguka juu ya kuwa mmoja wa wamiliki wa lebo ya Kings Music, ambayo yeye mwenyewe pia inamsimamia.

Akizungumza na www.eatv.tv, Abdu Kiba amesema kwamba yeye pia ni mmiliki wa Kings Music lakini aliamua kusimamiwa na lebo hiyo, ili aweze kuwapika vizuri vijana wenzake.

"Ukizungumzia Kings Music kuna King na Young King, mimi ndio young king, hii ni yangu mimi, na hawa ni vijana wangu, nimeamua kuwa ndani ya Kings Music kwa sababu nahitaji vijana wangu pia wafike kama nilipo mimi, hii ni yangu, mimi sina mkataba Kings Music, ningeamua pia ningekuwa boss”, amesema Abdu Kiba.

Lebo ya Kings Music mpaka sasa ina wasanii wanne, ambao ni yeye mwenyewe Abdu Kiba, K-2ga, Cheed, na Killy.