
Wachezaji wa Simba, kutoka kushoto ni Adam Salamba, Meddie Kagere na Pascal Wawa.
Klabu ya soka ya Yanga imewashangaza wengi kwenye dakika za mwisho baada ya kuwachukua nyota kadhaa huku pia ikitangaza kuwaacha wengine ambao walitegemewa huenda wangepewa nafasi ndani ya kikosi.
Wachezaji walioachwa na Yanga ni Godfrey Mwashiuya aliyekwenda Singida United, Obrey Chirwa aliyetimkia Misri na Donald Ngoma aliyekwenda Azam FC.
Mabingwa watetezi Simba walifanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo Hassan Dilunga pamoja na kumwongeza mkataba kiungo Said Hamis Ndemla na tayari nyota hao wameshatua nchini Uturuki ambako timu hiyo imeweka kambi.
Mchezaji wa Yanga Feisal Salum
Kikosi cha Yanga
Makipa: Klaus kindoki, Benno Kakolanya, Kabwili Ramadhani na Youthe Rostand Walinzi: Abdallah Shaibu, Kelvin yondan, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Andrew vicent na Pato Ngonyani. Viungo: Papy kabamba, Thaban kamusoko, Jafary Mohammed, Mohammed Issa Banka, Raphael Daud, Pius Buswita, Maka Edward, Feisal Salum 'Fei Toto', Deus kaseke, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi, S aid Mussa na Said Makapu Washambuliaji: Matheo Anthony, Mrisho Khalfan Ngassa, Amis Tambwe, Ibrahim Ajibu, Heriter Makambo, Yusuph Muhilu na Paul Godfrey.
Kikosi cha Simba
Makipa: Aishi Manula, Deogratius Munishi na Ally Salim. Walinzi: Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Mohammed Hussein, Nicolas Gyan, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, James Kotei, Yusufu Mlipili, Paul Bukaba, Vicent Costa na Salim Mbonde. Viungo: Jonas Mkude, Mzamiru Yasin, Shiza Kichuya, Cletus Chama, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga, Mohammed Ibrahim, Marcel Kaheza, Abdul Hamis, Rashid Juma na Said Ndemla. Washambuliaji: Emanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Adam Salamba na Mohammed Rashid.