Jumanne , 25th Dec , 2018

Ikiwa ni siku ya Krismasi leo watu mbalimbali wameungana na familia, marafiki, ndugu na jamaa kusherehekea sikukuu hiyo ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo huku msanii Lady Jay Dee akiwazodoa baadhi ya watu walioshinda mtandaoni.

Kushoto ni Lady Jay Dee na kulia ni msosi ambao leo umesindikiza sikukuu yake.

Kupitia mtandao wa Twitter mkali huyo wa 'Vocals' amewaambia watu ambao leo wapo sana mtandaoni huenda kwao hakuna sikukuu hivyo yeye anajiweka sawa na akishiba ndio atakuja mtandaoni kwa kasi.

''Watu wanaoshinda sana leo Twitter ujue kwao hakujapikwa na hakuna sikukuu. Mimi leo na Tweet kwa nadra, nikishiba ndio nitakuja kwa kasi jioni'', ameandika.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameendelea kutaniana na Lady Jay Dee wengine wakimwambia kuwa wanaoshinda mtandaoni hawajui kupika jambo ambalo limemfanya Jide aweke picha ya msosi ambao amekula.