Lulu afunguka ndoa yake kufungwa kimya kimya

Jumatano , 17th Apr , 2019

Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) ameelezea juu ya tetesi za yeye kufunga ndoa kimya kimya na mpenzi wake Francis Siza (Majizzo).

Lulu akiwa na mpenzi wake Majizo.

Akizungumzia suala hilo Lulu amesema kuwa habari hizo hazina ukweli na harusi yao itakuwa ya kawaida kama watu wengine, akisisitiza kuwa hakutokuwa na haja ya kuficha wala kufunga kwa siri.

"Mimi na mume wangu mtarajiwa tutafunga ndoa ya kawaida kabisa kama zilivyo harusi nyingine, tutakuwa na familia pamoja na ndugu na jamaa", amesema Lulu.

Mwanadada Lulu mwishoni mwa mwaka jana alivishwa pete ya uchumba na siku kadhaa baadaye alitolewa mahari na mchumba wake huyo na kinachosubiriwa hivi sasa ni harusi yao.