Madaha: Bado nipo Candy 'N' Candy

Jumatatu , 4th Mei , 2015

Baby Madaha, staa wa muziki ambaye ujio wake mpya katika game ni kupitia video mpya ya kolabo aliyofanya na Bella na Dully Sykes inayokwenda kwa jina la Mimi, amefafanua kuwa yeye bado ni 'First Lady' wa lebo ya Candy N Candy ya nchini Kenya.

msanii wa bongofleva nchini Baby Madaha

Baby Madaha amesema kuwa atakuwa kwenye lebo hiyo mpaka mwezi wa 9 ambapo mkataba wake utaisha rasmi.

Aidha mashabiki wake wengi wanashindwa kuelewa anafanya vipi kazi zake sasa, akiwataka kujua kuwa, ataachana na lebo hiyo baada ya kupima imemsaidia vipi ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Vilevile staa huyo akatumia nafasi hii kuweka wazi endapo kuharibika kwa mahusiano aliyokuwa nayo na boss wa lebo hiyo, ndiyo yaliyochangia yeye kujiweka mbali nayo, tofauti na zamani.