Jumamosi , 3rd Sep , 2016

Makundi matano leo yamefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya mchuano mkali wa makundi kumi kuonesha uwezo wa hali ya juu, katika hatua ya nusu fainali leo, na hatimaye matano yakatangazwa kushinda kuingia hatua ya fainali.

Kundi la Makorokocho lilipokuwa kazini shindano la Dance100% hatua ya nusu fainali.

Shindano la Dance100% hatua ya nusu fainali limefanyika katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki.

Akizungumza na EATV baada shindano hilo Jaji Super Nyamwela, amesema makundi yote yameonesha uwezo wa hali ya juu ila majaji wamezingatia vigezo na masharti ambavyo vimeweza kusaidia kupatikana makundi hayo matano.

“Makundi mengi yamefanya vizuri ila lazima alikuwa apatikane mshindi, hivyo tumeangalia mambo ya msingi kama tulivyowaelekeza na aliyeshindwa kukidhi vigezo tumeweza kutoa alama kulingana na namna walivyokuwa wanacheza ndipo mwisho wa siku tukapata haya matano bora kwa leo” Amesema Super Nyamwela.

Makundi yaliyofanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Dance100% 2016 ni haya yafuatayo.

BBK Boys

Team Makorokocho

Wazawa Crew

Clever Boys

D.D.I Crew

Makundi ambayo yameaga mashindano ya Dance100% mwaka huu wa 2016 ni haya yafuatayo.

J. Combat Crew kutoka Zanzibar.

Mazabe Poweder

The Quest Crew

Tatanisha Crew

The Heroes Crew

Shindano la Dance100% linadhaminiwa na Vodacom na Coca Cola na linaoneshwa na EATV Pekee siku ya Jumapili saa moja jioni.

BBK Crew
Tags: